Friday, July 28, 2017

YALIYOJIRI KWENYE MBIO ZA MWENGE WA UHURU WILAYANI KALIUA 23-24, JULAI 2017


Mwenge wa Uhuru uliwasili eneo la makabidhiano kijiji cha usindi wilayani kaliua
Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru baina ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo na Mkuu wa Wilaya ya Kaliua
Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilayani Kaliua na kukimbizwa umbali wa Km 115 katika vijiji 7 Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amezindua, ameweka mawe ya Msingi, na kutembelea miradi 8 mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya Sh 3,256,131,000 kwa mchanganuo ufuatao:-Halmashauri ya Wilaya Sh 100,056,000Serikali Kuu Sh 1,339,000,000 na jamii Sh 1,817,075,000.
Shiriki Kukuza Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu”. Ujumbe huu mahsusi ulitiliwa mkazo na kiongozi wa Mbio za Mwenge taifa dhidi ya;
  • Mapambano dhidi ya dawa za kulevya, tuwajali na tuwasikilize watoto na vijana,
  • Tuungane kwa pamoja dhidi ya rushwa kwa maendeleo, amani na usalama wa Taifa letu,
  • Tanzania bila maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na UKIMWI, inawezekana, Shiriki kutokomeza
  • Malaria kabisa kwa manufaa ya Jamii.


MSAFARA WA MWENGE WA UHURU ULIANZIA KIJIJI CHA USHOKOLA NA KUZINDUA MRADI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA MKAA MBADALA CHA NDUGU IDD HAMIS

Mradi huu umezinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwngw Wa Uhuru Kitaifa Bw Amour Hamad Amour 23, Julai 2017 mradi huu unatazamiwa kukuza uchumi wa vijana, kuongeza kipato, kutoa ajira, kuhifadhi mazingira kwa kupunguza ukataji wa miti holela na pia kusaidia katika kupunguza taka (mabaki ya mzao na vumbi la mbao) ambayo yote kwa pamoja yana madhara katika uhifadhi wa mazingira na afya ya jamii. Mradi huu umeweza kutoa ajira kwa vijana wapatao 6 wanaotoa huduma ya kukusanya taka ngumu, kutengeneza na kuanika mkaa, kuhifadhi na kuuza kwa watumiaji. Mradi huu ni jitihada  za kumuunga mkono Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Mradi huu unatarajiwa kuongezewa eneo na kuhamishiwa kwenye eneo lililotengwa na Halmashauri ya Wilya ya Kaliua kwa ajili ya viwanda vidogo (light Industries) na miradi ya vijana.
Posted On: July 24th, 2017


No comments:

Post a Comment