Sunday, September 10, 2017

ZIARA YA WAZIRI MKUU WILAYANI KALIUA


Katika ziara yake ya siku moja wilayani Kaliua iliyofanyika Augosti 11, Waziri Mkuu alipata fursa kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wafanyakazi wa halmashauri na kuhutubia mikutano ya hadhara.

Akizungumza na wafanyakazi wa wilaya ya Kaliua Mh. Majaliwa amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa ubununifu, uadilifu, uaminifu na kuhudumia  wananchi wote bila kujali itikadi zao.
Dhamira ya serikali ni kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi katika kila Nyanja, hivyo kila mfanyakazi hana budi kuwa na mpango mkakati wa kila siku ili tuweze kutekeleza filosofia ya Mh. Rais ya HAPA KAZI TU kwa vitendo”.
Pia Mh. Waziri Mkuu aliwaeleza wafanyakazi juu ya dhamira ya serikali ya kuboresha stahiki zao; ikiwemo kuwalipa madeni na kuahidi kuwa serikali iko mbioni kupandisha madaraja kwa wafanyakazi wanaostahiki.
Mh. Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji na Madiwani kwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato ya ndani ( katika mwaka 2016/17 halmashauri imekusanya 108% ya lengo ililojiwekea). Kwa upande mwingine Waziri mkuu amefurahishwa na usimamizi wa jengo la  Mkurugenzi wa Halmashauri na kuahidi kuiletea halmashauri pesa nyingene haraka kwa ajili kuendeleza miradi ya maji na barabara takriban kilometa 7 za hapa mjini Kaliua.
Katika mikutano ya hadhara aliyoifanya Ulyankulu na Kaliua Waziri Mkuu amekemea vikali juu ya Mauaji yaliyoifanya Kaliua kuongoza kitaifa jambo ambalo ni hatari na itadhoofisha ustawi kimaendeleo.
Kaliua ni wilaya ambayo inakua kwa kasi kimaendeleo haya serikali haitawavumilia wanaohusika na mauaji haya” alisema Waziri Mkuu na kutoa wito kwa wananchi kutunza mazingira na kusitisha uvamizi wa hifadhi kwani kwa sasa serikali inaendelea na zoezi la uhakiki wa mipaka ya vijiji na hifadhi na itatoa maelekezo pindi zoezi hilo litakapokamilika.
Kuhusu Tumbaku..
Tumbaku ni moja kati ya mazao makubwa matano ikiwemo kahawa, chai, pamba na korosho japokuwa wakulima wahawanufaiki kiuchumi.
“Serikali ya awamu ya tano imechukua hatua madhubuti katika korosho na tumefanikiwa. Sasa tumehamia katika tumbaku: tunaendelea kuwashughulikia wote waliokuwa wakiwahujumu wakulima na wengine tayari wapo ndani (rumande)” alisema.
Aliwaeleza wananchi kua kuanzia sasa bodi ya tumbaku na wetcu zimevunjwa na kutakua na wetcu mbili moja itakua karibu zaidi na wakulima wa Urambo na Kaliua na nyingine itashughulikia wilaya za Uyui, Sikonge na Nzega.
Pia kuanzia sasa ni marufuku tumbaku kununuliwa kwa dola kwa ni sehemu nyingine ambayo imewauiza wananchi kwa kiasi kikubwa. Sambamba na hilo ameonya walanguzi wa vishada kwa mauzo yote ya tumbaku yatafanyika katika AMCOS ambazo zitashirikiana kwa karibu na maafisa kilimo na maafisa ushirika tangu hatua za awali za kilimo.

No comments:

Post a Comment