Saturday, October 14, 2017

Wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wameanza mafunzo ya siku tatu ya mfumo wa upangaji mipango na bajeti ( PlanRep WEB) kuanzia leo tarehe 14/10/2017 hadi tarehe 16/10/2017. Mafunzo haya yatawajengea uwezo wakuu wa idara na vitengo katika uwajibikaji na upangaji wa mipango na bajeti za halmashauri. Kupitia mfumo huu Halmashauri itaokoa kiasi cha pesa kilichokuwa kikitumika katika uandaaji wa taarifa za mipango na bajeti kila mwaka kwa kuwa taarifa hizo zitakuwa zikiwasilishwa kielektroniki, hivyo kutoa wigo mpana kwa halmashauri kuelekeza nguvu katika kuwahudumia wananchi. Tembelea http://www.kaliuadc.go.tz/new/mafunzo-ya-planrep-web-kwa-wakuu-wa-idara-na-vitengo

No comments:

Post a Comment