Saturday, April 28, 2018

SHEREHE YA KUWAAGA WASTAAFUWastaafu wa Halmashauri ya wilaya Kaliua walioagwa katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kaliua kutoka Kushoto ni Mzee Peter Mabula (Ardhi), Rose Ntungi (Afya), Lilian Rubaba (Elimu), Theresia Nshimba(Afya), Alfred Msengi (Maendeleo ya Jamii) na Shabani Lenge (Kilimo) 

Afisa Utumishi-DHRO Bi Flora Malima akiwashuru wastaafu kwa ushirikiano walioonyesha katika kipindi chote wakiwa watumishi wa Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na kuwataka watumishi kuiga yaliyo mema kutoka kwao.
Bwana Abeid Mluge (Afisa Mifugo) akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wafanyakazi wa Halmashauri na kuwatakia wastaafu mapumziko mema nje ya Utumishi serikalini.

Dafroza Kabazu (kulia) mratibu wa sherehe akigawa bahasha zenye zawadi akiwapatia zawadi waagwa kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo. 

Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi mbalimbali kutoka kwa watumishi.

Bwana Jimmy Nkwamu Afisa Elimu Sekondari akimpatia zawadi maalum Bi Lilian ambae amestaafu utumishi katika idara ya Elimu.

Mzee Peter Mabula akitoa shukrani kwa Uongozi wa Halmashari ya Kaliua na watumishi wenzake kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake huku akiwaasa watumishi kudumisha nidhamu na upendo wakati wote.
Bwana Dickson Mhozya na MC wa sherehe akipokea keki kutoka kwa mstaafu wastaafu hakika ilikuwa furaha kubwa

Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Aristides Raphael akilishwa keki na Mstaafu kutoka idara ya Afya katika hafla ya kuwaaga waliokuwa watumishi kutoka idara mbalimbali
No comments:

Post a Comment