Saturday, May 12, 2018
Tuesday, May 1, 2018
SEMINA YA WATENDAJI WA VIJIJI
Saturday, April 28, 2018
SHEREHE YA KUWAAGA WASTAAFU
Wastaafu wa Halmashauri ya wilaya Kaliua walioagwa katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kaliua kutoka Kushoto ni Mzee Peter Mabula (Ardhi), Rose Ntungi (Afya), Lilian Rubaba (Elimu), Theresia Nshimba(Afya), Alfred Msengi (Maendeleo ya Jamii) na Shabani Lenge (Kilimo)
Afisa Utumishi-DHRO Bi Flora Malima akiwashuru wastaafu kwa ushirikiano walioonyesha katika kipindi chote wakiwa watumishi wa Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na kuwataka watumishi kuiga yaliyo mema kutoka kwao.
Bwana Abeid Mluge (Afisa Mifugo) akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wafanyakazi wa Halmashauri na kuwatakia wastaafu mapumziko mema nje ya Utumishi serikalini.
Dafroza Kabazu (kulia) mratibu wa sherehe akigawa bahasha zenye zawadi akiwapatia zawadi waagwa kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo.
Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi mbalimbali kutoka kwa watumishi.
Bwana Jimmy Nkwamu Afisa Elimu Sekondari akimpatia zawadi maalum Bi Lilian ambae amestaafu utumishi katika idara ya Elimu.
Mzee Peter Mabula akitoa shukrani kwa Uongozi wa Halmashari ya Kaliua na watumishi wenzake kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake huku akiwaasa watumishi kudumisha nidhamu na upendo wakati wote.
Bwana Dickson Mhozya na MC wa sherehe akipokea keki kutoka kwa mstaafu wastaafu hakika ilikuwa furaha kubwa
Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Aristides Raphael akilishwa keki na Mstaafu kutoka idara ya Afya katika hafla ya kuwaaga waliokuwa watumishi kutoka idara mbalimbali
Tuesday, April 24, 2018
MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2018 WILAYANI KALIUA
Watumishi wa halmashauri ya Kaliua wakiwa wamependeza katika sare za mwenge kutoka kushoto ni Hazina, Clara, Dafroza, Mwanahamisi na Leah.
Kutoka kushoto ni Dickson Mhozya cashier Halmashauri ya wilaya ya Kaliua akiwa na Maafisa tarafa wa Ulyankulu na Kaliua Gavana Mswazi na Gavana Mahenge.
...endelea zaidi
Sunday, February 18, 2018
ZIARA YA ALAT MKOA WA TABORA MWAKA 2018
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Haruna Kasele na Mkurugenzi Mtendaji Dr. John Pima wakionyesha cheti cha mshindi wa Kwanza ALAT 2018
Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Tabora wakiwa katika Kikao kilichofanyi katika ukumbi wa Halmashauri wilayani Kaliua
Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Tabora Mh. Adam Malunkwi akiongoza ujumbe wa ALA 2018 kwa walipomtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kaliua
Friday, December 15, 2017
ZAIDI YA MITI 5,000 KUPANDWA WILAYANI KALIUA
>>Mkuu wa Wilaya Kaliua ashiriki kupanda miti barabara ya KALIUA - KIGOMA leo.....bofya hapa
>>Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakipanda miti eneo la STENDI MPYA .....bofya hapa
ZOEZI LA UPANDAJI MITI WILAYANI KALIUA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dr. John Pima akipanda mti katika zahanati ya Kaliua
Dr. John Marco Pima akitoa maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya Kaliua namna bora ya upandaji wa miti.
Afisa Tarafa wa tarafa ya Kaliua Ndugu Bethod Mahenge, akishiriki vyema katika zoezi la upandaji miti katika zahanati ya Kaliua
Katibu Tawala-DAS wa Wilaya ya Kaliua akishiriki zoezi la upandaji miti katika zahanati ya Kaliua
Dr. Aristides Raphael (kulia) Mganga Mkuu wa Wilaya akiwa na Afisa Mapato wa Halmashauri wakishirikiana kupanda miti katika zoezi lililofanyika kwenye zahanati ya Kaliua.
Tuesday, October 17, 2017
MAFUNZO YA SIKU TATU MFUMO WA UPANGAJI MIPANGO NA BAJETI YAHITIMISHWA HAPO JANA TAREHE 16 Oktoba 2017
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Ndugu John Pima, akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya mfumo wa PlanRep kabla ya kuyafunga hapo jana. Soma Hotuba
Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua - DPLO Ndugu Edwin Mashala, akitoa taarifa ya mafunzo ya PlanRep kwa Mkurugenzi Mtendaji muda mchache kabla ya kufungwaa kwa mafunzo hayo Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo Ndugu Marco Kapela.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo wakiwa katika mazoezi ya vitendo ya matumizi ya mfumo wa upangaji bajeti wa PlanRep.
Tuesday, August 8, 2017
KILELE CHA MOANYESHO YA NANE-NANE 2017
Mkurugenzi Mtendaji Dr. John Marco Pima akionyesha cheti mara baada ya kutangazwa mshindi...bonyeza hapa kusoma zaidi
Wananchi mbalimbali wakijifunza namna bora ya uzalishaji wa tumbaku ambalo ni moja ya chanzo kikubwa cha mapato wilaya ya Kaliua
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mh. Haruna Kasele akisaini kitabu baada ya kuwasili katika banda la maonyesho ya wilaya ya Kaliua
Mkurugenzi Mtendaji Dr. John Pima akikagua bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika banda ya wilaya ya Kaliua kwenye maonyesho ya nane nane
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwasili kuadhimisha kilele cha maonyesho ya nane nane 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)