Tuesday, May 1, 2018

SEMINA YA WATENDAJI WA VIJIJI

Muhasibu wa halmashauri ya wilaya kaliua  akitoa mafunzo kwa watendaji wa vijiji

watendaji wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wakufunzi

Saturday, April 28, 2018

SHEREHE YA KUWAAGA WASTAAFU



Wastaafu wa Halmashauri ya wilaya Kaliua walioagwa katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Kaliua kutoka Kushoto ni Mzee Peter Mabula (Ardhi), Rose Ntungi (Afya), Lilian Rubaba (Elimu), Theresia Nshimba(Afya), Alfred Msengi (Maendeleo ya Jamii) na Shabani Lenge (Kilimo) 

Afisa Utumishi-DHRO Bi Flora Malima akiwashuru wastaafu kwa ushirikiano walioonyesha katika kipindi chote wakiwa watumishi wa Serikali na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua na kuwataka watumishi kuiga yaliyo mema kutoka kwao.
Bwana Abeid Mluge (Afisa Mifugo) akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wafanyakazi wa Halmashauri na kuwatakia wastaafu mapumziko mema nje ya Utumishi serikalini.

Dafroza Kabazu (kulia) mratibu wa sherehe akigawa bahasha zenye zawadi akiwapatia zawadi waagwa kwa niaba ya kamati ya maandalizi ya sherehe hiyo. 

Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea zawadi mbalimbali kutoka kwa watumishi.

Bwana Jimmy Nkwamu Afisa Elimu Sekondari akimpatia zawadi maalum Bi Lilian ambae amestaafu utumishi katika idara ya Elimu.

Mzee Peter Mabula akitoa shukrani kwa Uongozi wa Halmashari ya Kaliua na watumishi wenzake kwa ushirikiano waliompatia katika kipindi chote cha utumishi wake huku akiwaasa watumishi kudumisha nidhamu na upendo wakati wote.
Bwana Dickson Mhozya na MC wa sherehe akipokea keki kutoka kwa mstaafu wastaafu hakika ilikuwa furaha kubwa

Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Aristides Raphael akilishwa keki na Mstaafu kutoka idara ya Afya katika hafla ya kuwaaga waliokuwa watumishi kutoka idara mbalimbali




Sunday, February 18, 2018

ZIARA YA ALAT MKOA WA TABORA MWAKA 2018

Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Haruna Kasele na Mkurugenzi Mtendaji Dr. John Pima wakionyesha cheti cha mshindi wa Kwanza ALAT 2018


Wajumbe wa ALAT Mkoa wa Tabora wakiwa katika Kikao kilichofanyi katika ukumbi wa Halmashauri wilayani Kaliua


Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Tabora Mh. Adam Malunkwi akiongoza ujumbe wa ALA 2018 kwa walipomtembelea Mkuu wa Wilaya ya Kaliua

Friday, December 15, 2017

ZAIDI YA MITI 5,000 KUPANDWA WILAYANI KALIUA



>>Mkuu wa Wilaya Kaliua ashiriki kupanda miti barabara ya KALIUA - KIGOMA leo.....bofya hapa


>>Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakipanda miti eneo la STENDI MPYA .....bofya hapa

ZOEZI LA UPANDAJI MITI WILAYANI KALIUA

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dr. John Pima akipanda mti katika zahanati ya Kaliua
 Dr. John Marco Pima akitoa maelekezo kwa watumishi wa Halmashauri ya Kaliua namna bora ya upandaji wa miti.
 Afisa Tarafa wa tarafa ya Kaliua Ndugu Bethod Mahenge, akishiriki vyema katika zoezi la upandaji miti katika zahanati ya Kaliua

Katibu Tawala-DAS wa Wilaya ya Kaliua akishiriki zoezi la upandaji miti katika zahanati ya Kaliua
Dr. Aristides Raphael (kulia) Mganga Mkuu wa Wilaya akiwa na Afisa Mapato wa Halmashauri wakishirikiana kupanda miti katika zoezi lililofanyika kwenye zahanati ya Kaliua.

Tuesday, October 17, 2017

MAFUNZO YA SIKU TATU MFUMO WA UPANGAJI MIPANGO NA BAJETI YAHITIMISHWA HAPO JANA TAREHE 16 Oktoba 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Ndugu John Pima, akiwahutubia washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya mfumo  wa PlanRep kabla ya kuyafunga hapo jana. Soma Hotuba

Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua - DPLO Ndugu Edwin Mashala, akitoa taarifa ya mafunzo ya PlanRep kwa Mkurugenzi Mtendaji muda mchache kabla ya kufungwaa kwa mafunzo hayo Kulia ni Mwenyekiti wa Mafunzo Ndugu Marco Kapela.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo wakiwa katika mazoezi ya vitendo ya matumizi ya mfumo wa upangaji bajeti wa PlanRep.

Tuesday, August 8, 2017

KILELE CHA MOANYESHO YA NANE-NANE 2017

Mkurugenzi Mtendaji Dr. John Marco Pima akionyesha cheti mara baada ya kutangazwa mshindi...bonyeza hapa kusoma zaidi


Wananchi mbalimbali wakijifunza namna bora ya uzalishaji wa tumbaku ambalo ni moja ya chanzo kikubwa cha mapato wilaya ya Kaliua

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mh. Haruna Kasele akisaini kitabu baada ya kuwasili katika banda la maonyesho ya wilaya ya Kaliua
Mkurugenzi Mtendaji Dr. John Pima akikagua bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika banda ya wilaya ya Kaliua kwenye maonyesho ya nane nane
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwasili kuadhimisha kilele cha maonyesho ya nane nane  2017